Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Nkasi Afraha Hassan amesikiliza kero za watumishi wote wa halmashauri ya wilaya Nkasi na kuzipatia ufumbuzi .
Kikao kazi hicho ambacho kimewajumuisha watumishi wa kada mbalimbali wa halmashauri hiyo ambacho kiliketi kwenye ukumbi wa Community Centre leo Novemba 15,2024 ambapo mkurugenzi mtendaji wa wilaya alipata fursa ya kusikiliza kero zote ambapo nyingi ziliweza kutafutatiwa ufumbuzi.
Baada ya kuzisikiliza kero hizo na nyingi kuzipatia ufumbuzi mkurugenzi mtendaji aliwasihi watumishi hao kupendana na kufanya kazi kwa weredi na kuleta ufanisi katika halmashauri ya wilaya Nkasi
Sambamba na hayo amewataka Watumishi hao kufuata sheria ,kanuni na taratibu za kazi pindi wanapotimiza majukumu yao ya kazi na kuahidi kushughulikia changamoto na kero za watumishi pindi zinapojitokeza huku akiwasisitiza na kuwashauri watumishi kuachana na tabia ya majungu na kusemana na badala yake wajishughulishe na fursa mbalimbali ambazo zinapatikana katika Hamashauri hiyo ili kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Bw.Raineli Mwenda amewakumbusha watumishi kuzingatia sheria kanuni taratibu za kazi na kuwa na nidhamu ya kazi pindi wanapotimiza majukumu yao ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwahi kazini na kutoka kazini muda uliopangwa.
Vilevile Bw.Mwenda ametoa rai kwa watumishi wote Halmashauri ya Nkasi kuendelea kujifunza kwa bidii mfumo wa PEPMIS ambapo zoezi la kuingiza malengo katika mfumo bado linaendelea na kuwataka kutekeleza zoezi hilo likamilike kwa wakati.
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki