UTANGULIZI
Idara ya Afya ni miongoni mwa idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Idara ya Afya inatekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo mbalimbali inayotolewa na Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Huduma hizi zimekuwa zikitolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya na kwa njia ya mkoba katika maeneo mbalimbali ya Wilaya. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kuna jumla ya vituo 45 vya kutolea huduma za afya. Vituo hivi vinamilikiwa na serikali, watu binafsi, mashirika ya dini pamoja na taasisi za serikali. Vituo vya kutolea huduma za Afya vinavyomilikiwa na serikali ni 15, Vituo 21 vinamilikiwa na watu binafsi, 4 vinamilikiwa na mashirika ya dini na vituo 5 vinamilikiwa na taasisi za serikali. Kati ya vituo hivyo 45, kuna hospitali 1, vituo vya Afya 12 na zahanati 32.
Idara ya Afya inatekeleza majukumu makuu mawili abayo ni Afya kinga na Afya tiba. Kupitia Afya tiba idara imelenga kutoa matibabu sahihi kwa gharama nafuu kwa wananchi wa Wilaya pamoja na Wilaya za jirani. Afya kinga imelenga kuwakinga wananchi wasipate magonjwa yale ya kuambukiza, yasiyoyakuambukiza pamoja na kuzuia magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.
Idara imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na kutekeleza mpango mkakati wa afya wa V wa mwaka 2015 -2020. Katika kuhakikisha wananchi wanapata tiba sahihi, idara imekuwa ikitekeleza majukumu yafuatayo:
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki