Kuratibu shughuli zote za usimamizi wa uendelezaji Miji, upangaji wa Miji, Upimaji wa Ardhi, uthaminishaji na umilikishwaji kwa mujibu wa sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 na sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya mwaka 2007.
Idara ya Mipango Miji na Ardhi hutoa huduma kwa wananchi kupitia vitengo vyake vikuu vinne;-
KITENGO CHA MIPANGOMIJI.
Kuratibu shughuli zote za usimamizi wa uendelezaji Miji katika Manispaa ya Ilemela. Usimamizi na uendelezaji Miji unahusisha upangaji wa matumizi ya Ardhi na urasimishaji wa makazi yasiyo rasmi.
Kutoa elimu na ushauri kwa jamii kuhusu uendelezaji Miji kwa mujibu wa sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya mwaka 2007.
KITENGO CHA ARDHI.
Kusimamia masuala yote ya ardhi, uaandaaji wa hatimiliki, uhamisho wa miliki, na utatuzi wa migogoro ya ardhi. Aidha siku ya Jumanne kila wiki ni siku ya kusikiliza migogoro ya ardhi kwenye Kata kwa ratiba inayoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali ikiwemo kodi ya pango la ardhi (Land Rent).
Huduma kwa wananchi ni kwa siku za Jumatatu na Ijumaa kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 8.00 mchana.
KITENGO CHA UTHAMINI.
Kinashughulikia masuala yote ya uthamini, ikiwemo uthamini kwa ajili ya fidia, uthamini kwa ajili ya kodi za majengo, uthamini kwa ajili kubadili miliki na ukadiriaji wa kodi ya majengo, Ardhi pamoja na malipo ya mbele ya ardhi. (Premium), uthamini kwa ajili ya dhamana, uthamini kkwa ajili ya kuongeza muda wa kumiliki hati (Renewal).
KITENGO CHA UPIMAJI NA RAMANI.
Kinashughulikia shughuli zote za upimaji wa ardhi na uandaaji wa ramani za upimaji (Survey plans)