Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ina misitu ya asili 15 inayokadiriwa kuwa na ukubwa wa hekta 3,014 na pia kuna mito mikubwa na midogo isiyokauka kwa kipindi chote cha mwaka. Misitu hii ina aina mbalimbali za miti zinazotoa maua yanayowezesha upatikanaji wa asali yenye ubora wa kipekee. Hata hivyo yapo mazao mbalimbali ya chakula na biashara kama mahindi, alizeti, viazi vitamu na miti mingi ya matunda ambayo hutoa maua yanayosaidia katika upatikanaji wa poleni.
Hata hivyo katika kuhakikisha kuwa rasilimali ya nyuki inaendelezwa ili ichangie katika kuinua kipato cha jamii na kushiriki katika utunzaji wa mazingira endelevu, huduma mbalimbali zinatolewa kwa wananchi. Huduma hizo ni pamoja na :- Utoaji wa hamasa na elimu ya ufugaji wa nyuki, Kutoa vifaa vitumikavyo katika ufugaji wa nyuki, ikiwemo mizinga ya kisasa na mavazi ya kurinia kwa vikundi vya wafugaji wa nyuki, Kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi vya wafuga nyuki.
Hadi mwezi February/2015, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ina mizinga ya kisasa ya ufugaji nyuki ipatayo 1,363 ya kisasa na 4,648 ya kienyeji na wafugaji wa nyuki wapatao 357 na idadi hii inazidi kuongezeka kutokana na hamasa inayoendelea kutolewa.
UFUGAJI WA NYUKI
Ufugaji wa nyuki ni taaluma inayotumia rasilimali ya nyuki (wanaouma na wasiouma) na mimea katika kuzalisha asali, nta, gundi ya nyuki, maziwa ya nyuki, majana, sumu ya nyuki, chavua na nyuki wenyewe.
FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI
Mdau wa ufugaji wa nyuki anaweza kufaidika na taaluma hii kama vile:-
FURSA ZA UFUGAJI NYUKI ZILIZOPO
CHANGAMOTO ZINAZOKABILI KITENGO CHA NYUKI
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki