Sunday 22nd, December 2024
@Wilaya ya Nkasi
Wilaya Nkasi mkoani Rukwa imejipanga kwa ajiri ya kuupokea Mwenge wa Uhuru mwaka huu na miradi yenye zaidi ya shilingi bilioni moja inatarajia kuzinduliwa
Akitoa taarifa kwenye kikao cha kamati ya Mwenge cha Wilaya Mkuu wa Wilaya Nkasi Mh. Said M. Mtanda amesema mpaka sasa maandalizi yote ya awali yamekamilika na kuwa Mwenge huo wa Uhuru utawasili wilayani Nkasi April 7 na mkesho wa Mwenge utakua katika kata ya Kirando
Mwenge huo utapokelewa katika kijiji cha Kizi ukitokea Mkoani Katavi na kuanza kukimbizwa Wilayani Nkasi ambapo utakwenda Lyazumbi, Paramawe, Mwai, Mkole na Ipanda.
Baada ya hapo Mwenge huo wa Uhuru utakimbizwa mjini Namanyere katika eneo la Majengo, Isunta, Nkomolo, Masolo, Katongoro na Kirando utakakofanyika mkesha wa Mwenge na kesho yake Mwenge huo utakibidhiwa Wilayani Kalambo katika Kijiji cha Katuka
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki