Friday 20th, September 2024
@KIRANDO
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Charles Makongoro Nyerere kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Peter Amblose Lijualikali pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nkasi Ndg. Valeriana Ackimu Mwapasi alizindua Kliniki ya kutatua matatizo ya Wanachi ambayo kimkoa yalifanyika katka kijiji cha Kirando kilichopo Halmashauri ya Nkasi. Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alisikiliza Matatizo Mbalimbali ya Wananchi wa Kirando na Kuyapatia ufumbuzi. Hii ni kutokana na maagizo Mh. Raisi Mama Samia Suruhu Hassan ambeye aliagiza Viongozi wa Serikali katika ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na Vijiji kwenda kwa Wannchi kusikiliza Matatizo yao na Kuyatatua, zoezi hili litafanyika kati ya 21/02/2024 mpaka 31/03/2024.
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki