Sunday 22nd, December 2024
@KITUO CHA AFYA NKOMOLO
Katibu tawala wilaya ya Nkasi Ndg. Cosmas Kuyela ameongoza Wananchi na watumishi wa taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali katika kuimarisha usafi wa Mazingira kwenye vituo vya kutolea huduma za afya Wilayani Nkasi ikiwa ni kuelekea katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 61 uhuru.
Maadhimisho hayo yatafanyika disemba 9 mwaka huu 2022,ambapo katika wilaya ya Nkasi maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru yataenda sambamba na mdahalo mkubwa utakaohusisha Makundi mbalimbali ikiwemo Vijana na wazee yatakayojadili kwa pamoja Mabadiriko ya kimaendeleo kabla na baada ya uhuru hususani katika wilaya ya Nkasi na Mkoa wa Rukwa kwa Ujumla.
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki