Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi kupitia jeshi la zima moto na uokoaji imetoa mafunzo ya kujikinga na moto kwa watumishi wa makao makuu wa Halmashauri hiyo wawapo katika mazingira mbalimbali yakiwemo ya kazi.
Aidha lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa kwa watumishi hao juu ya matumizi sahihi ya vyazo vya moto, pamoja na kupunguza na kizuia ajali na vifo vitokanvyo na Moto.
Akizungumza katika mafunzo hayo Staff Sajenti Ciprian Mhuvi, ambaye pia ni kaimu Afisa Zima moto wilayani Nkasi, aliainisha visababishi vya moto( vyanzo )katika mazingira mbalimbali kuwa ni uzembe: unaosababishwa na uvutaji holela wa Sigara pamoja na mapishi jikoni, hitilafu ya umeme inayosababishwa na kuzidisha mzigo kwenye vifaa vya umeme ( Extension Cable), kuunga umeme kienyeji, kutokukagua mifumo ya umeme ambapo amebainisha kuwa ni muhimu Kila baada ya miaka mitatu mifumo ya umeme ikaguliwe katika majengo mbalimbali ili kupunguza na kizuia madhara yanayoweza kujitokeza.
Sambamba na hayo aliongeza kuwa, matumizi ya vifaa vya umeme kwa muda mrefu ikiwemo Runinga, Redio, swichi mbovu, uandaaji wa mashamba kwa kuchoma moto na uwindaji ni miongoni mwa vyanzo vya moto vinavyoweza kuleta madhara makubwa katika jamii.
Kupitia mafunzo hayo Staff Sajenti Mhuvi, alisema zipo hatua madhubuti za kuchukua ili kujikinga na moto katika mazingira mbalimbali ikiwemo mahala pa kazi, ambazo ni kutoa elimu kwa umma, kufanya ukaguzi kwenye vyombo vya usafiri na usafirshaji, kuzingatia matumizi sahihi ya vifaa vya umeme, kuwa na vifaa vya kuzimia moto, mapishi salama pamoja na kuzingatia ujenzi bora hasa kwa kutumia malighafi yenye uwezo wa kizuia Moto kuanzia nusu saa hadi dakika arobaini na tano.
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki