Serikali wilayani Nkasi imewakabidhi pikipiki aina ya Boxer Watendaji wa kata 9 zilizopo wilayani hapa,pikipiki hizo zimekabidhiwa leo Machi 10.2023 katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Nkasi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Ndugu Pancras Maliyatabu amesimamia zoezi la ugawaji wa pikipiki huku akisisitiza vyombo hivyo vya usafiri kutumika kama ilivyokusudiwa ili kuharakisha utendaji pale changamoto za usafiri zinapojitokeza.
kupitia hafla hiyo nae Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri William Mwakalambile amewataka watendaji wa kata hizo 9 kuhakikisha wanaongeza na kuboresha ukusaji wa mapato kwani pikipiki hizo zitawasadia katika ufuatiliaji wa kina katika ukusanyaji,watendaji wa kata waliopewa pikipiki ni pamoja na kata za Kala,Sintali,Kate,Myula,Isale,Kipande,Nkandasi,Mkwamba, na Mtenga.
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki