Kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya Nkasi ndugu Ladislaus Mzelela leo julai 13 amefungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wajasiriamali hususani Makundi ya wanawake na vijana na washiriki wengine katika mafunzo hayo ni pamoja na Watendaji wa kata na vijiji kwa kata za Nkomolo,Majengo,Namanyere na Kipundu Mafunzo yaliyratibiwa na ofisi ya mkurugenzi mtendaji kupitia idara ya maendeleo ya jamii.Mzelela amewataka washiriki wote kutambua umuhimu wa mafunzo hayo kwani lengo lake ni kusaidia wanavikundi na wajasiriamali kutoka katika maeneo mbalimbali kujikwamua kiuchumi hasa kwa kurasimisha shughuli wanazozifanya ili zitambulike na serikali.Mada mbalimbali zimefundishwa ikiwemo suala la uwezeshaji katika kupata mikopo ya mitaji kupitia taasisi mbalimbali za kibenki ikiwemo benki ya CRDB ambao nao ni washirika wameeleza fursa watakazopata wajasiriamali baada ya kurasimisha vikundi vyao.Amesisitiza kuwa ili kukuza mtaji ni lazima kuwe na nidhamu katika matumizi ya fedha pia amewataka wajasiriamali kutambua umuhimu wa kuwa na leseni za biashara pamoja na kutunza kumbukumbu za kibiashara kwani kufanya hivyo ni rahisi kukua kibiashara.Serikali wilayani nkasi inajukumu la kuhakikisha wajasiriamali wanatafutiwa masoko ya bidhaa zao pale wanapojisajiri na kutambuliwa kupitia idara ya maendeleo ya jamii.Kupitia mafunzo hayo pia imetolewa elimu ya kuzingatia viwango na ubora wa bidhaa hasa zinazotokana na ujasiriamali,matumizi sahihi ya leseni za biashara, upatikanaji na utunzaji wake.Afisa lishe kutoka ofisi ya mganga mkuu wa wilaya alipata nafasi ya kutoa elimu ya lishe pamoja na taarifa ya kuanzishwa kwa siku ya lishe ya kijiji itakayofanyika kila mwaka.Mfumo wa maisha ya kisasa na Wazazi kujikita zaidi kwenye shughuli za kiuchumi kunapelekea kupunguza malezi sahihi kwa Watoto kinachopelekea kuwepo kwa vitendo vya kikatili katika jamii.Amesema kuwa kama Watoto watapata malezi na stahiki zao sahihi kuna uwezekano mkubwa wa kulindwa na kuepukana na vitendo vya kikatili ambavyo kwa sasa vimeshamiri katika jamii.
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki