Wafugaji kupitia umoja wao wa Wafugaji wilayani Nkasi mkoani Rukwa wameshauriwa kuunda ushirika utakaowawezesha kujenga mtaji mkubwa na kuweza kuanzisha kiwanda cha kuchakata bidhaa mbalimbali zitokanazo na mazao ya mifugo na kuweza kujikwamua kiuchumi.
Ushaurio huo umetolewa jana na afisa ushirika wa mkoa Rukwa Wales Kilia kwenye mkutano mkuu wa umoja wa Wafugaji wilayani Nkasi ambapo alidai kuwa Wafugaji katika umoja wao huo wanao uwezo mkubwa wa kuanzisha ushirika mkubwa utakaowawezesha kutengeneza mtaji mkubwa na kugeuka na na kuwa wawekezaji kupitia viwanda.
Alisema katika taarifa aliyosomewa na katibu wa umoja umoja huo jinasa Bilia ni kuwa umoja huo wenye wanachama 159 kwa muda wa miaka mitatu iliyopita walikua na hakiba ya Tshs,Mil.12 lakini hadi kufikia sasa wameweza kufikisha Mil.35 na kuwa mtiririko huo kama wataugeuza umoja huo na kuwa ushirika wanaweza wakafika mbali zaidi.
Alisema katika taarifa hiyo ameona kipengele ambacho wafugaji wameiomba serikali kuwatafutia wawekezaji na kuwa sasa wao wenyewe wanaweza wakawa wawekezaji kwa kuanzisha kiwanda kikubwa ambacho mwisho wa siku kitawatoa katika lindi la umasikini ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira kwa vijana wao.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tatu imejielekeza kwenye uchumi wa kati ambao ni wa viwanda na kuwa jambo hilo linawezekana kama wao wataweza kujenga ushirika wenye nguvu na kuwa ushirika utawafanya wao waweze kukopesheka kwenye taasisi mbalimbali za kifedha na kuwa viwanda ni kitu cha kawaida ambacho kinaweza kikaanzishwa na mtu yeyote na kuondoa mawazo kuwa wawekezaji pekee ndiyo wenye uwezo wa kuwekeza viwanda.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Nkasi Julius Kaondo kwa upande wake aliwatoa wasiwasi wafugaji hao juu ya uanzishwaji wa ushirika na kuwa yeye sasa atawasaidia Wafugaji hao walau kuweka kituo cha kukusanyia maziwa ili wanunuzi waweze kuwakuta hapo na hata ikibidi atamfuata mwekezaji wa kuwekeza katika sekta hiyo ya Maziwa ambalo ni moja ya mazao yatokanayo na mifugo yao.
Alisema kuna baadhi ya changamoto nyingi ambazo serikali inabidi izifanyie kazi na kuwa amezisikia na zile alizo na uwezo nazo atahakikisha anazitafutia ufumbuzi wa haraka
Mwenyekiti wa umoja huo Msemakweli Msalaba alidai kuwa wazo hilo wamelichukua na kuwa watalifanyia kazi haraka sana na kuhakikisha kuwa wanaanzisha ushirika mkubwa na wenye nguvu ambao pia utakua ni wa kupigiwa mfano.
Na aliiomba serikali iwe inatoa elimu kwa wafugaji juu ya matumizi bora ya ardhi,ikiwa ni pamoja na namna ya kuitumia mifugo waliyonayo katika kuweza kujiletea maendeleo badala ya kuona fahari ya kuishi nas mifugo mingi isiyokuwa na tija
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki