Wanachama wa Bank za VICOBA wametakiwa kuendesha vikundi vyao kwa kufuata katiba na misingi waliyojiwekea na hiyo ndiyo siri kubwa ya kuweza kudumisha vikundi hivyo.
Wito huo umetolewa jana na meneje wa bank ya NMB tawi la Nkasi mkoani Rukwa Leonida Domician kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Tushikamane Vicoba ambapo amedai kuwa ili kuweza kufanikiwa kwa vikundi hivyo vya VCOBA ni lazima misingi ile iliyowekwa ifuatwe na kuwa hiyo ndiyo silaha kubwa ya kuweza kujipatia mafanikio.
Amesema kuwa VICOBA ni Bank ndogo ambazo zinawawezesha wanachama kuweka na kukopa na kuwa vikundi vingi vimekuwa vikishindwa kuendelea kwa kutofuata misingi hasa la nidhamu kwenye marejesho na kuwa kinachotakiwani kusimamiwa kwa misingi ya kikatiba waliyojiwekea na kuwa taasisi nyingi za kifedha zimekuwa zikivurugana sana hasa pale marejesho yanapokuwa magumu na kwa kuozingatia kanini.
Sambamba na hilo alikipongeza kikundio hicho cha VICOBA kwa kufanikiwa kutengeneza mtaji wa Tshs,Mil.40 na kudumu kwa muda wa miaka mitatu bila ya kuteteleka na kuwa huo ni mwanzo mzuri kwao na wakiendelea hivyo huenda wakatengeneza mtaji mkubwa na wanachama wakaweza kujikwamua kiuchumi kuanzia ngazi ya familia
Mwenyekiti wa Tushikamane Vicoba Marry Siame amesema kuwa kikundi chao cha vicoba kilianza kikiwa na watu wachache ambao ni Watumishi wa halmashauri na kuwa waliendelea kupata wanachama wengi na kuweza kufanikisha kuunda vikundi vingine viwili vyenye wanachama 30 kila kimoja ambavyo ni Tumaini Vicoba na Tujisogeze.
Amesema kuwa Vicoba hivyo vimekuwa vikipata mafanikio makubwa kutokana na nidhamu kubwa waliyoijenga katika umoja wao na kuwa wamekua wakijengewa uwezo mkubwa wa kiuendeshaji kutoka katika taasisi ya UYACODE ambayo imekuwa ikiwajengea uwezo kila mara na kuwasaidia kukabiliana na changamotop ambazo zimekua zikijitokeza.
Baadhi ya wanachama wamedai kuwa toka wajiunge na vicoba hivyo kwa kiasi kikubwa hata maisha yao yamebadilika sana kutokana na mikopo ya mara kwa mara inayopatikana katika vikundi hivyo
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki