Watumishi wa Serikali wanaoiwakilisha halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mkoani Tanga 2025, leo wameshiriki mashindano ya riadha ya mita 100(SHIMISEMITA) ambapo washiriki wawili kwa wanaume wameibuka washindi wa pili ambao ni Mgeta Turo na Selemani Kapinga huku mshindi kwa wanawake nafasi ya tatu akiibuka Leticia Mwanamwene.
Mashindano hayo yanafanyika leo Agosti 21, 2025 katika viwanja vya Tanga school ikiwa ni moja ya michuano inayoshindaniwa katika michezo mbalimbali Mkoani humo.
Afisa utamaduni, sanaa na michezo bw. Lusekelo Swedy amesema kuwa amefurahishwa na kiwango cha wawakilishi wa wilaya hiyo na kuwahamasisha watumishi wengine kushiriki michezo mbalimbali ili kuiwakilisha vyema halmashauri, hata hivyo ameshukuru uongozi wa halmashauri kwa kuwawezesha kushiriki michuano hiyo.
Ikumbukwe mashindano hayo yalianza Agosti 15, 2025 na kikomo itakuwa Agosti 29, 2025, halmashauri 140 zinashiriki mashindano hayo lengo likiwa ni kuwaleta pamoja watumishi nchini nakukuza ushirikiano.
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki