Watu wazima ambao hawakufanikiwa kupata elimu kupitia mfumo rasmi wametakiwa kuichangamkia fursa ya elimu inayotolewa nchini kote bila kujali umri wao na aibu, kwani upo utaratibu mzuri wa wao kufundishwa.
Hayo yamebainishwa leo September 2, 2025, na mkuu wa wilaya ya Nkasi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi, katika sherehe za kilele Cha maadhimisho ya wiki ya elimu ya watu wazima Peter Ambrosi Lijualikali, zilizofanyika katika viwanja vya chuo Cha VETA Paramawe Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa ,huku akitoa wito kwa watu wote kuishika elimu na kuipigania.
Aidha katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 29, mwaka huu Lijualikali amewasisitiza wananchi kudumisha amani umoja na mshikamano kama taifa pamoja na kufanya kampeni kistaarabu.
"Nafahamu hapa wengi mmejiandikisha na zoezi lilifanyika vizuri nafahamu, Kila mtu ana chama chake, tunawagombea mbalimbali kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na urais, ombi langu kwenu nikuendelea kudumisha amani umoja na mshikamano kama taifa tukafanye kampeni za kistaarabu, tukawafanyie tunaowataka lakini pia tukawaheshimu tusiowataka" amesema Lijualikali.
Awali akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi Afisa elimu ya watu wazima Sekondari na elimu nje ya mfumo rasmi Thomas Mhagama kwa niaba ya Afisa elimu ya watu wazima Msingi na nje ya mfumo rasmi Jesca Lwiza amesema kuwa chimbuko la maadhimisho ya elimu ya watu wazima yalianza mwaka 1975, ambapo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliona ni vyema watu wake wapate elimu kwani idadi kubwa kwa wakati huo walikuwa hawajui kusoma Wala kuandika.
Kupitia taarifa hiyo Mhagama amesema Tanzania kama ilivyo nchi nyingine duniani imekuwa ikiadhimisha juma la elimu ya watu wazima Kila mwaka shabaha yake kuu ni kuhamasisha jamii nzima kutambua nafasi ya elimu kwakila mtu bila kujali umri, jinsia na hali ya maisha, na hii ikidhihirisha kuwa elimu ni endelevu na haina kikomo na ni urithi wakudumu kwamaendeleo ya mtu binafsi na Taifa kwa ujumla.
Akisoma hotuba kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Nkasi, mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Afraha Hassani amesema kuwa dhana ya kukuza kisomo katika dhama za kidigitali imekuja kwasababu katika maisha kwenye jamii , mazingira yamebadilika, hali ya hewa imebadilika, mifumo ya Kiuchumi imebadilika, hali ya milipuko ya magonjwa inaongezeka nakudai kuwa vyote hivi vinaitaka jamii iendelee kusoma ili kupata elimu ya kukabiliana navyo bila kujali utoto hadi utu uzima, hivyo jamii ibadilike iendane na sayansi na Teknolojia.
Aidha alifurahishwa na mwamko mkubwa wa vyuo wilayani Nkasi katika kushiriki maadhimisho ya wiki ya elimu ya watu wazima ambayo yameletwa mwamko mkubwa kwa jamii kwenda kujifunza.
" Nimefurahi kuona mwamko mkubwa wa vyuo vyetu wilayani Nkasi kuja kushiriki maadhimisho haya ya wiki ya elimu ya watu wazima ambayo kimsingi yameletwa mwamko kwa jamii kuja kujifunza" alisema mkurugenzi huyo.
Sambamba na hayo ameagizi Kila Kijiji na kitongoji ambacho kina watu wazima wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu, kuhakikisha madarasa ya watu wazima yanafunguliwa, na kusisitiza kua wanafunzi waliocha shule kwa sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito warudi shule kuendelea na masomo ili watimize ndoto zao.
Maadhimisho hayo ya kilele cha wiki ya elimu ya watu wazima yalipambwa na maonesho ya fani mbalimbali kutoka katika vyuo na taasisi za serikali na zisizo za serikali huku yakisindikizwa na kaulimbiu isemayo " kukuza kisomo katika zama za kidigitali kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu"
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki