KIKAO CHA KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI CHAJADILI TAARIFA ZA ROBO YA PILI KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025.
Katika kudhibiti maambukizi ya ukimwi nchini Halmashauri ya wilaya ya Nkasi imekaa kikao chake cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Lengo likiwa ni kujadili na kupitisha rasimu na mpango wa bajeti wa mwaka wa fedha 2026/2027.
Kikao hicho kilichofanyika leo January 23, 2026 katika ukumbi wa ofisi ya Mkurugenzi, kilijadili na kupitisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na nusu mwaka 2025/2026 na mapendekezo ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Mbali na taarifa hizo kikao kilijadili taarifa za utekelezaji wa idara kwa robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki