SHULE BORA YAWEZESHA MAFUNZO YA UWAWA WILAYANI NKASI.
Mradi wa wa Shule Bora kwa kushirikiana na UK Aid Wametoa mafunzo ya Ushirikishwaji wa walimu na Wazazi (UWAWA) pamoja na Uongozi wa shule ikiwa ni awamu ya kwanza kwa Wenyeviti wa kamati za shule, maafisa elimu kata na walimu wakuu wa shule za elimu awali na msingi zilizopo katika kata za Kala,Wampembe,,Kizumbi,Ninde,Mkinga,Kipili,Kirando,Itete,Korongwe,Kabwe,Sintali,Mkwamba na Ntuchi.
Lengo la mafunzo haya ni kuimarisha ushirikiano na mfumo mzuri wa mawasiliano kati ya wazazi na walezi walimu,wanafunzi na jamii pia mafunzo haya yatasaidia kuimarisha miundombinu jumuishi na mazingira salama ya ujifunzaji ikiwa ni pamoja na matumizi ya zana na uhamasishaji wa jamii kuchangia upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi.
Shule Bora ni Mradi wa Serikali unaofadhiliwa na UK aid. Mradi unaotekelezwa katka mikoa tisa ya Tanzania bara ikiwemo na mkoa wa Rukwa
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki