Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndg. William Mwakalambile Leo tarehe 18/08/2023 amepokea POS 8 kutoka Shirika la The Nature Concervancy Shirika linalofanya kazi ya utunzaji sahihi wa Mazalio ya Samaki Mwambao mwa ziwa Tanganyika.
Mwakalambile akipokea POS hizo ofisini kwake amesema kuwa POS hizo 8 zitaongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato katika vijiji 8 vilivyopo mwambao mwa ziwa Tanganyika aidha amewataka watendaji katika maeneo zitakapopelekwa POS hizo kuzitumia kwa uaminifu mkubwa na kuzingatia utunzaji wake ili zitumike kulingana na malengo yaliyokusudiwa.
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki