Mkuu wa wilaya Nkasi Peter Lijualikali amekutana na kufanya mazungumzo na Wadau wa Afya wakiwemo wataalamu,Wazee maarufu,Wachungaji wa makanisa mbalimbali,Madiwani na viongozi wa vyama vya siasa,ambapo kupitia kikao hicho amesisitiza kila mmoja kuchukua tahadhari mapema juu ya ugonjwa wa EBOLA kwani wilaya ya Nkasi ipo Mpakani mwa Nchi zinazotajwa kuwa na Wagonjwa wa ugonjwa huo wa EBOLA.
Lijualikali amesema”Watu wa usalama tayari wanamajukumu yao,Watumishi wa mungu na wadau wengine ndani ya wilaya yetu ni jukumu letu kuhakikisha tunatoa elimu na kuhamasisha wananchi wachukue tahadhari”.
Nae mratibu wa Magonjwa ya dharura wilayani Nkasi Dkt Katutu amesema Wizara ya afya imeelekeza kila wilaya kuweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo. Ugonjwa wa EBOLA unaenezwa kwa kugusa nguo ,shuka au godoro kugusa majimaji ya mwili kama vile mkojo, kamasi ,kinyesi ,kamasi, mate, damu matapishi na jasho njia nyingine ni kuchangia vitu vyenye ncha kali na kusa wanyamapori au mizoga ya wanyama kama vile nyani na swala wanaoripotiwa kubeba virusi vya EBOLA.
Dkt Katutu amesema dalili za ugonjwa wa EBOLA ni pamoja na kua na homa kali ya ghafla, kuumwa kichwa , maumivu ya misuli, kutapika ,mwili kuwa dhaifu, kuhara damu ,kutokwa na damu sehemu za wazi jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo ni kuepuka kushika nguo shuka au godoro kugusa majimaji ya mwili kama vile mkojo, kamasi ,kinyesi ,kamasi, mate, damu matapishi na jasho ya mtu mwenye ugonjwa wa EBOLA kuepuka kushika wanyama pori wakiwa hai au mizoga,kunawa mikono mara kwa mara na kutozika wa kugusa maiti ya mtu aliyefariki akiwa na dalili hizo.
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki