BARAZA LA WAFANYA KAZI NKASI LA KETI KATIKA KIKAO CHAKE CHA KWANZA.
Baraza la wafanya kazi wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa leo January 22, 2026, limefanya kikao chake cha kwanza cha kujadili na kupitisha rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027, kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Awali akifungua kikao hicho Mwenyekiti, ambae pia ni kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Nkasi Bw.Eliud Njogellah, alisema bajeti hiyo ni shirikishi hasa kupitia baraza la wafanya kazi ambao wanawakilisha Idara mbalimbali, ili kuhakikisha malengo ya Halmashauri yanatimia.
Aidha kupitia kikao hicho wajumbe wa baraza la wafanya kazi wilaya, walipokea taarifa ya utendaji kazi wa Halmashauri kwa kipindi cha kuanzia January 2025 hadi Desemba 2025, pamoja na taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa Mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025, 2025/2026 na mapendekezo ya mpango na bajeti kwa Mwaka 2026/2027.
Sambamba na hayo miongoni mwa machache Kati ya mengi yaliyoshauriwa na wajumbe kupitia kikao hicho, ni pamoja na uboreshwaji wa miundombinu kuwa rafiki kwa watu wenye mahitaji maalum kwa sehemu zote zinazotolewa huduma za jamii, pamoja na usimamizi wa maadili kwa watoto, kwani wengi wao wanaathiriwa kitaaluma kwa kuangalia filamu almaarufu kama season kwenye vibanda vya video na hata majumbani kwao.
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki