Serikali wilayani Nkasi mkoani Rukwa imeteketeza TANI mbili ya samaki
wakavu waliobainika kuhifadhiwa kwa kutumia sumu kinyume na sheria ya
Mamlaka ya chakula na dawa TFDA Na,30(1)a,b,c ya mwaka 2003.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya Nkasi Missana Kwangula ni kuwa walipata taarifa
kutoka kwa raia wema juu ya kufanyika kwa vitendo hivyo haramu vya
mfanyabiashara Dernest Batupu wa kijiji cha Kalungu kata ya mkinga
kuwahifadhi samaki wake kwa kutumia sumu ili samaki hao wasiweze kuoza
na kuwa dawa hiyo ni hatari sana kwa afya ya watumiaji wa samaki hao
Amedai kuwa baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo alihojiwa na kukubali
kuwa anatumia sumu katika kuwahifadhi samaki wake ili wasiweze
kuharibika kwa maana anawapeleka mbali kibiashara nchini Burundi.
Kwangula amefafanua kuwa baada ya hapo na kufuatia uchunguzi wa
kitaalamu chini ya TFDA kufanyika na kubaini kuwapo kwa sumu katika
samaki hao walichukua hatua ya kumtoza faini ya shilingi milioni moja
kwa mujibu wa sheria chini ya TFDA na mhusika kuridhia samaki hao
kuteketezwa kitu ambacho kimefanyika leo
Mganga mkuu wa wilaya Hashimu Mvogogo amesema kuwa samaki
wanaohifadhiwa kwa kutumia sumu wana hatari kubwa ya kiafya kwa
watumiaji wa samaki hao na kuwa msako mkali utaendelea ili kuweza
kuwabaini wale wote wanaofanya vitendo hivyo
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki