Mwenge wa Uhuru unatarajia kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Nkasi yenye thamani ya zaidi Tshs,Bil.29
Mwenge huo unatarajia kukimbizwa wilayani Nkasi april 10 ya mwaka ukiwa umebeba ujumbe mahususi wa ‘maji ni haki ya kila mtu ,tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.
Akizungumza kwenye kikao cha maandalizi ya mapokezi ya Mwenge Mkuu wa Wilaya Nkasi Said Mtanda amesema miradi itakayozinduliwa ni ya sekta mbalimbali kama Maji, Elimu, Afya, kilimo, Ujasiliamali, Barabara na mingine mingi, na kuwa miradi hiyo mpaka sasa imekamilika katika kiwango cha kuridhisha.
Mkuu huyo wa wilaya amedai kuwa kwa mwaka huu wa 2019 lengo kuu la wilaya ni kutaka kufanya vizuri katika mapokezi ya mwenge kitaifa na kuwa, kwa Mkuu yeyote wa Idara ambaye mradi wake utakataliwa ni uzembe na kuwa atakamata papo hapo na Polisi
Alidai kuwa haoni sababu za wilaya Nkasi kushindwa kufanya vizuri katika mbio za mwenge na kuwa kila mkuu wa idara ni lazima ahakikishe mradi wake umekaa vizuri na kuwa kitendo cha mradi kukataliwa ni uzembe ambao yeye hatakubaliana nao.
Wajumbe wa kamati ya mwenge kwa upande wao wamemuahidi mkuu wa wilaya kuwa katika mbio za mwenge mwaka huu watafanya vizuri kwa maana ya kwamba wamejipanga ipasavyo kuhakikisha ushindi katika ukimbizaji wa mwenge kwa mwaka huu unapatikana
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki