Madaktari bingwa kutoka Italia wapatao 32 watafika wilayani Nkasi na
kutoa tiba kwa wagongwa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa wilaya Nkasi Said Mtanda
ni kuwa madaktari hao wataletwa hapa wilayani na serikali kwa
kushirikiana na taasisi ya Mvimwa na kuwa madaktari hao wakifika
watawekwa kwenye kambi moja na watu wenye shida watakwenda moja kwa
moja kuwaona madaktari hao bingwa.
Amesema kuwa baada ya muda madaktari hao watapelekwa katika
hospitali mbalimbali za serikali wilayani Nkasi na kwenda kutoa tiba
katika hospitali hizo ili wananchi waweze kunufaika na wataalamu hao.
Lakini pia amesema kuwa kufuatia ushirikiano huo mzuri wa serikali ya
wilaya na taasisi ya MVIMWA Madaktari wetu kutoka wilaya Nkasi
watapelekwa Italia kwenda kupata kozi fupifupi za kitabibu ili kuweza
kuwaimarisha zaidi katika eneo hilo la tiba.
Amedai kuwa madaktari hao kutoka Italia watakua watakua wanaishi kwa
muda wa miezi mitatu wanarudishwa italia na wengine wanakuja na kuwa
katika eneo hilo la afya kuna uwezekano mkubwa wa kuwa tija katika
siku za usoni
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki