Baadhi ya viongozi wa dini na viongozi wa Kimila wilayani Nkasi mkoani Rukwa wamelalamikia kitendo cha kupuuzwa kwa baadhi ya mila na desturi kuwa ni miongoni mwa sababu zinazochangia ongezeko la mimba za utotoni wilayani humo.
Kauli hiyo wameitoa leo kwa nyakati tofauti wakati wakichangia katika kikao cha siku moja kilichoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Plan International nawakutanisha viongozi hao katika ukumbi wa Ngunga kwa lengo la kuweka mikakati ya kukabiliana na ndoa pamoja na mimba za utotoni wilayani humo.
Akichangia mada katika kikao hicho mmoja wa wazee wa mila Yacinta Kasandala amesema kuwa zipo baadhi ya mila na desturi zilizokuwa nzuri na zikikua zikizuia watoto wakike kujihusisha na mapenzi kabla ya ndoa lakini siku hizi zimepuuzwa kitendo kinachosababisha watoto hao kupata mimba katika umri mdogo.
Naye sheikh mkuu wa wilaya ya Nkasi Hadhir Daluesh amesema kuwa hivi sasa hofu ya mungu imepungua hali ambayo hata maadili yamepungua na kusababisha watoto wa kike na kiume kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo mapenzi ambapo bado viongozi wa dini wanakazi kubwa ya kukemea vitendo hivyo.
Awali akifungua mkutano huo mratibu wa mradi wa kuzuia ndoa za utotoni wilayani Nkasi kutoka shirika la Plan International Nestory Frank alisema kuwa kikao hicho kimefanyika ili kuwakutanisha viongozi hao na kuwajengea uwezo katika kupambana na ingezeko la mimba za utotoni kwakuwa wananafasi kubwa ya kuzungumza na kusikilizwa na wazazi.
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki