IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
Utangulizi
Idara ya Mifugo na Uvuvi yenye jumla ya watumishi 21 imegawanyika katika sekta ya Mifugo ambayo ina watumishi 14 na sekta ya Uvuvi watumishi 7.
Shughuli zinazofanywa na Idara ya Mifugo na Uvuvi
1.0 Idadi ya mifugo
Kufuatia sensa ya mifugo iliyofanyika mwaka 2016/2017 Wilaya ilikuwa na idadi ya mifugo kama ifuatavyo: ng’ombe 176,565 (wa maziwa 31 kutoka ranchi ya Kalambo na 6 Kilangala mission); mbuzi 42,210; kondoo 27,173; nguruwe 3,896; punda 1,647; mbwa 10,841; kuku 75,503; bata 5,814 na farasi 14. Aina ya ng’ombe zilizopo Wilayani ni Santa gertruids, Simmental, Borani, Frisian, Fipa na Tarime.
Ng’ombe aina ya Santa gertruids ilikuwa nafasi ya kwanza Kitaifa mwaka 2011 katika mashindano ya wafugaji wadogo wa ng’ombe wa nyama
Ng’ombe aina ya Boran ilikuwa nafasi ya kwanza Kitaifa mwaka 2012 katika mashindano ya wafugaji wadogo wa ng’ombe wa nyama
2.0 Uwiano wa mifugo na eneo la malisho
Hadi kufikia mwaka 2016/2017 eneo la malisho linalomilikiwa na wafugaji ni Ha 79,312 sawa na 16.42% ya Ha 483,000 zinazofaa kwa malisho Wilayani. Maeneo hayo ni yale ambayo pia hutumika kwa kilimo nyakati za masika na malisho kipindi cha kiangazi. (Sensa ya mifugo, 2016/2017).
3.0 Miundombinu ya mifugo na uvuvi
Miundombinu iliyopo Wilayani inayomilikiwa na Serikali ni majengo 7 ya machinjio ndogo za mifugo; karo 1; bucha 11 za nyama ya ng’ombe, mbuzi na kondoo; majosho 16 ya ng’ombe, mbuzi na kondoo; vibanio 4, malambo 2, kliniki 3 za mifugo zinazoendelea na ujenzi, minada 3 ya awali ya mifugo na majosho 16 ya kuogeshea mifugo. Aidha miundombinu mingine inayomilikiwa na wafugaji wenyewe ni majosho 10, vibanio 6 na mabirika 5. Aidha miundombinu ya uvuvi ni mwalo wa samaki Kirando, soko la samaki Korongwe. Pia kuna jumla ya idadi mabwawa ya kufugia samaki 34 kata za Namanyere, Nkomolo, Mkwamba, Mtenga, Chala, Kizumbi na Kirando.
Ukanda wa ziwa Tanganyika Wilaya ya Nkasi una urefu wa kilometa 186 wenye jumla ya Kata 10 ambazo ni Kabwe, Korongwe, Kirando, Itete, Kipili, Mkinga, Ninde, Kizumbi, Wampembe na Kala. Sekta hii inachangia asilimia 28.01 ya makisio ya mapato ya ndani Tshs 644,394,000/= ya Halmashauri kupitia leseni za vyombo vya uvuvi, leseni za wavuvi, ushuru wa samaki na dagaa katika mwaka wa fedha 2016/2017.
4.0 Mafanikio
Nkasi District Council
Anwani ya posta: P. O. Box 2, Namanyere - Nkasi
Simu: +255252830006
Simu ya mkononi: +255252830006
Barua pepe: ded@nkasidc.go.tz
Haki miliki